Proverbs 8:22-31


22 aBwana aliniumba mwanzoni mwa kazi yake,
kabla ya matendo yake ya zamani;
23 bniliteuliwa tangu milele,
tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa.
24 cWakati hazijakuwepo bahari, nilikwishazaliwa,
wakati hazijakuwepo chemchemi zilizojaa maji;
25 dkabla milima haijawekwa mahali pake,
kabla vilima havijakuwepo, nilikwishazaliwa,
26 ekabla hajaumba dunia wala mashamba yake
au vumbi lolote la dunia.
27 fNilikuwepo alipoziweka mbingu mahali pake,
wakati alichora mstari wa upeo wa macho
juu ya uso wa kilindi,
28 gwakati aliweka mawingu juu
na kuziweka imara chemchemi za bahari,
29 hwakati aliiwekea bahari mpaka wake
ili maji yasivunje agizo lake,
na wakati aliweka misingi ya dunia.
30Wakati huo nilikuwa fundi stadi kando yake.
Nilijazwa na furaha siku baada ya siku,
nikifurahi daima mbele zake,
31 inikifurahi katika dunia yake yote
nami nikiwafurahia wanadamu.
Copyright information for SwhNEN